1. Muachie ujumbe wa kimahabba nyumbani katika
eneo asilolitarajia
2. Anapojipulizia manukato mwambie kuwa harufu yake ni
nzuri
3. Mshukuru kwa huduma za nyumbani hata kama ni
kidogo.
4. Msifu kwa mapishi yake na umwambie unavyoyahusudu.
Usifanye hivyo mkiwa mezani, fanya baada ya kumaliza kula.
5. Iwapo kuna kifaa kimeharibika nyumbani
kitengeneze
6. Usifu uzuri wa nywele zake
7. Mkumbatie unapomkuta amehuzunika.
8. Msaidie kuondokana na wasiwasi.
9. Amiliana naye kwa huruma na upole anapokuwa katika
siku zake
10. Shiriki katika kumfanya aonekane mzuri, hata kwa
kumpendekezea nguo ya kuvaa.
11. Anzisha mazungumzo kuhusu upendo na mahabba
12. Mpe zawadi yenye kumkumbusha kuhusu wewe.
13. Mbusu kila unapoenda kazini
14. Mpatie msaada pindi anapouhitaji
15. Mshirikishe katika kufanya maamuzi.
16. Usimpe sababu za kumpa huzuni.
17. Mpe remote atazame filamu anayoipenda.
18. Mtegee sikio anapozungumza.
19. Usiwasifu wanawake wengine mbele yake.
20. Shirikiana naye katika michezo anayoipenda
21. Usiache kuwa karibu naye kimwili
22. Muite kwa majina matamu
23. Muombe radhi unapomkosea
24. Mchekeshe
25. Siku ya ndoa yenu ifanye kuwa siku muhimu sana
26. Mweleze wazi matatizo yanayokukabili
27. Usimlazimishe kufanya mapenzi kama hana utayari na
hamu ya kufanya.
0 comments:
Post a Comment