Kwa uchache watu 29 wamepoteza maisha na wengine
70 kujeruhiwa katika mlipuko uliotokea kwenye soko la fataki nchini Mexico.
Mlipuko huo umetokea kwenye soko la fataki la San
Pablito katika mji wa Tultepec, kilometa 32 kaskazini mwa mji mkuu Mexico City.
Idadi ya vifo inaweza kuongezeka kwa kuwa vikosi vya
uokozi vinaendelea kuwatafuta waathirika katika eneo la mlipuko.
Askari wa zimamoto wakitembea katiktai ya vifusi vilivyoachwa na mlipuko uliotokea kwenye soko la fataki nchini Mexico Desemba 20, 2016. |
Wanajeshi wamepelekwa eneo hilo ili kusaidia kuwahamisha
na kuwapeleka majeruhi hospitalini kwa magari ya wagonjwa na helikopta.
Gavana wa jimbo la Mexico, Eruviel Avila, amesema
kipaumbele kwa sasa ni kuwahudumia majeruhi.
Askari wa zimamoto akitembea katikati ya kifusi kilichosababishwa na mlipuko mkubwa kwenye soko la fataki nchini Mexico , Desemba 20, 2016. |
"Sauti ya milipuko ilianza kurindima nasi tulidhani
kuwa ni kwenye warsha ya eneo jirani," mwananchi mmoja wa eneo hilo
alinukuliwa na shirika la habari la AFP. "Majirani walisema kuwa walihisi
kila kitu kinatikisika, lakini mimi sikubaini hilo kwa sababu nilikuwa nakimbia,"
alisema.
0 comments:
Post a Comment