“Kuanzia leo na kuendelea, tukiwa na nia ya kutekeleza
wajibu wetu wa kimataifa wa Mkataba wa Geneva wa mwaka 2006 ambao Burundi
iliusaini, nchi yetu itahama hatua kwa hatua kutoka kwenye matangazo ya
analogia kwenda kwenye digitali”, amesema Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza katika
hotuba yake aliyoitoa katika sherhr ya uzinduzi wa matangazo ya televisheni kwa
mfumo wa digitali kwenye ofisi za Televisheni ya Taifa la Burundi leo asubuhi
ya tarehe 19 Desemba 2016, kama ilivyoripotiwa na mtandao wa IWACU.
Rais huyo aliomba radhi kwa serikali yake kushindwa
kuhamia mfumo wa matangazo ya digitali tarehe 17 Juni 2015, ambayo ndiyo
iliyokuwa tarehe ya mwisho.
Waziri wa mawasiliano, habari na teknohama wa nchi hiyo,
Nestor Bankumukunzi, alisema kuwa maendeleo hayo yamefikiwa kutokana na mkopo
kutoka Benki ya Exim ya China na ahadi ya ving’amuzi iliyotolewa na China.
Mabadiliko hayo yatakuwa ya hatua kwa hatua yakianza na
Mkoa wa Bujumbura, eneo la katikati mwa nchi na hatimaye kuenea nchi nzima.
Aidha, Rais wa Burundi alizindua utandazaji wa
miundombinu ya Mkongo (Fiber Optics) kwa eneo la Bujumbura, hatua itakayosaidia
kupatikana kwa mawasiliano ya kasi katika taasisi za serikali kama vile Ikulu,
Bunge, Seneti, hospitali na mahakama.
0 comments:
Post a Comment