Balozi wa Urusi nchini Uturuki, Andrey Karlov, akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho ya sanaa mjini Ankara Uturuki Desemba 9, 2016. Balozi huyo ameuawa kwa kupigwa risasi. |
Balozi wa Urusi nchini Uturuki, Andrey Karlov, amefariki
dunia baada ya kupigwa risasi na mtu asiyejulikana wakati alipokuwa akizinduia
maonesho ya sanaa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Ankara.
Mshambuliaji huyo aliuawana kikosi maalum kwenye eneo
hilo la Wilaya ya Çankaya katikati mwa Ankara.
Balozi Karlov alipelekwa hospitalini baada ya kupigwa
risasi mara nane ambapo watu wengine kadhaa walijeruhiwa.
Maafisa wa serikali ya Urusi wamesema kuwa shambulizi
hilo lilifanywa na mtu mwenye siasa na mtazamo mkali.
Picha ikimuonesha muuaji wa Balozi wa Urusi nchini Uturuki akiwa amemsimamia baada ya kumpiga risasi balozi huyo wakati wa ufunguzi wa maonesho ya sanaa mjini Ankara Uturuki, Desemba 19, 2016. |
"Wakati balozi akitoa hotuba, mtu mmoja mrefu
aliyevalia suti alianza kupiga risasi juu kisha akamlenga balozi,” amesema
shuhuda mmoja. “Alisema kitu fulani kuhusu ‘Aleppo’ na ‘kisasi’.”
Picha zilimuonesha mtu huyo aliyevalia suti nyeusi akiwa
ameshika bastola na amesimama jirani na eneo la kutolea hotuba ambalo kuta zake
zilikuwa zimetundikwa picha mbalimbali. Watu wanne akiwemo mtu aliyeonekana
kuwa balozi, walikuwa wamelala sakafuni.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Urusi, Maria
Zakharova, amesema katika taarifa iliyorushwa kwenye televisheni kuwa wizara
yake itatoa tamko kuhusu shambulizi dhidi ya balozi huyo.
Taarifa zaidi itawajia hapa hapa....
0 comments:
Post a Comment