OBAMA: TUMEPELEKA ASKARI 275 IRAQ

 

Rais Barack Obama amesema kuwa askari 275 wa Kimarekani wamepelekwa nchini Iraq ili kuulinda ubalozi wa Marekani na raia wake nchini humo.

Mapema Jumapili wizara ya mashauri ya kigeni ya nchi hiyo ilitangaza kitumwa kwa kikosi hicho lakini haikutaja ukubwa wake.

Katika barua yake kwa uongozi wa bunge la Congress, Rais Obama amesema kuwa kuanzia Juni 15 askari hao walianza kusambaa kwenye maeneo mbalimbali ya Iraq kwa lengo la kuwalinda wafanyakazi wa Kimarekani na ubalozi wake mjini Baghdad.

Aidha, Rais Obama ameashiria kuwa kikosi hicho kitaendelea kubaki Iraq kadiri itakavyohitajika.


Leo Rais Obama anatarajiwa kufanya kikao na jopo lake la masuala ya usalama kudurusu hali ya kuzorota kwa usalama nchini Iraq, kuangalia hatua inayopaswa kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kufanya mashambulizi ya ndege kuwazuia wanamgambo wanaoishikilia miji kadhaa mashariki mwa Iraq.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment