AMCHINJA MKE NA WATOTO KABLA YA KWENDA KUTAZAMA MECHI YA UINGEREZA NA ITALIA




Shabiki mmoja wa soka anatuhumiwa mchinja mkewe na watoto wake wawili na kisha kwenda na marafiki zake kuangalia mechi ya soka kati ya Uingereza na Italia kwenye klabu moja ya usiku.

Miili ya mkewe, bi Cristina Omes mwenye umri wa miaka  38, na watoto wao, Giulia mwenye umri wa miaka 5 na Gabriele mwenye umri wa miezi 20, ilikutwa kwenye makazi yao katika eneo la Motta Visconti, jirani na mji wa Milan, nchini Italia.

Ripoti zinasema kuwa wote walikutwa wakiwa na majeraha mbalimbali huku shingo ya kila mmoja ikiwa imekatwa.

Carlo Lissi ambaye ni mtaalamu wa Computer ameshitakiwa kwa mauaji hayo.

Baada ya kuhojiwa kwa saa kadhaa, inadaiwa jamaa huyo mwenye umri wa miaka 31 alikiri kufanya mauaji hayo na kuwaambia polisi wampe adhabu kubwa kabisa.

Jamaa huyo aliwaambia polisi kuwa alifanya mauaji hayo Jumamosi usiku kwa sababu alikuwa amezama kwenye penzi la mwanamke mwingine.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment