Makamu wa Rais wa Argentina Amado Boudou ameitwa
mahakamani na kesi yake kusikilizwa kwa muda wa saa tano kwa tuhuma za kuhusika
ufisadi unaojumuisha kashfa ya na umiliki wa kampuni binafsi iliyoidhinishwa
kuchapisha vitabu vya benki. Ripoti zinaashiria kuwa jaji ana ushahidi wa
kutosha kumtia hatiani.
Kutokana na taathira ya kesi hii, maofisa wa serikali
walielezea matumaini yao kwamba jaji ataruhusu mwenendo wa kesi hiyo kuoneshwa
moja kwa moja na vituo vya televisheni.
Boudou alipowasili mahakamani, alilakiwa na maelfu ya
wafuasi wake, ambao wanadai kuwa tuhuma hizo ni sehemu ya kampeni ya vyombo vya
habari dhidi yake na kuivuruga serikali.
Baada ya kiongozi huyo kutoa ushahidi wake uliochukua
masaa kadhaa, Jaji Jorge Lijo hakutoa hukumu bali alitaka waitwe watetezi
wengine kutoa ushahidi zaidi kuhusu kadhia hiyo kabla ya kutoa uamuzi wa
mwisho.
Wakati bwana Boudou akiondoka mahakamani alitoa
ufafanuzi kuhusu mwenendo wa kesi hiyo. Uamuzi wa jaji umetoa nafuu kwa
serikali ya rais Cristina Fernandez de Kirchner. Kwa sasa mahakama ina siku 10
kabla ya kutoa uamuzi dhidi ya kesi hiyo na mustakbali wa Makamu huyo wa Rais
umegubikwa na giza nene.
0 comments:
Post a Comment