Mahakama nchini Bangladesh imewahukumu adhabu ya kifo
wanachama wanane wa chama cha Kiislamu baada ya kudaiwa kuhusika na shambulizi
la bomu la mwaka 2001 lililoua watu kumi.
Wakati akitoa hukumu hiyo leo, Jaji Ruhul Amin alisema
kuwa shambulizi hilo lilifanywa kwa lengo la kuivuruga nchi na kuzusha tafrani.
Alisema kuwa mkuu wa kundi lililopigwa marufuku la Harkat-ul-Jihad
al Islami (HUJI), Mufti Abdul Hannan, naye ni miongoni mwa washitakiwa.
Wanachama hao walishtakiwa kwa tuhuma za kutekeleza
shambulizi la bomu katika maadhimisho ya mwaka mpya wa Kibengali mwaka 2001 katika
mji mkuu wa nchi hiyo, Dhaka.
Aidha, mahakama hiyo imewahukumu adhabu ya kifo watu wengine
sita kwa tuhuma za kutekeleza mashambulizi mawili ya mabomu yaliyojeruhi watu
kadhaa.
Hata hivyo, wakili wa upande wa utetezi, bwana Faruque
Ahmed amesema kuwa washtakiwa walikiri kufanya makosa baada ya kushurutishwa na
kuadhibiwa na polisi wakati wa kuwahoji na ameahidi kukata rufaa.
0 comments:
Post a Comment