SERIKALI ya Gambia imetangaza kuwa inajitoa katika Jumuiya
ya Madola (Commonwealth), ikisema kuwa kamwe haitakuwa “mwanachama wa taasisi
yoyote ya ukoloni mamboleo.”
"Wananchi wanataarifiwa kuwa serikali ya Gambia
imejiondoa katika Mataifa ya Jumuiya ya Madola mara moja,” serikali ilisema
katika taarifa iliyotolewa jana Jumatano, kama ilivyoripotiwa na AFP.
"Serikali imejiondoa katika uanachama wa Jumuiya ya
Madola ya Uingereza na imeamua kuwa Gambia kamwe haitakuwa mwanachama wa
taasisi yoyote ya ukoloni mambo leo inayowakilisha kuendeleza ukoloni,”
iliongeza kusema taarifa hiyo.
Mpaka sasa haijajulikana wazi kitu gani kilichopelekea
uamuzi huo wa kushtukiza na wa kushtusha.
Jumuiya ya Madola ni mkusanyiko wa mataifa ambayo kwa
kiasi kikubwa yalikuwa makoloni ya Mwingereza, na ilianzishwa rasmi kwa Azimio
la London mwaka 1949.
AFP
0 comments:
Post a Comment