KUNDI la wapigaji wa al-Shabaab la nchini Somalia
limetishia kuongeza mashambulizi makali dhidi ya Kenya, siku chache baada ya kundi
hilo kuwaua makumi ya watu katika jengo moja la kibishara mjini Nairobi.
Wapiganaji wa al-Shabab wameapa kuigeuza miji ya Kenya kuwa
kile walichokiita kuwa ni viunga vya makaburi.
Katika taarifa yao walioitoa leo, wapiganaji hao
alisema:
"Tutawashambulia Wakenya mahala panapowaumiza
zaidi, tutaigeuza miji yao kuwa makaburi na mito ya damu itatiririka Nairobi”.
Taarifa hiyo imekuja baada ya Kenya kukataa kuyaondosha
majeshi yake nchini Somalia.
"Uamuzi wa serikali ya Kenya kutoviondoa vikosi
vyake Somalia ni dalili kwamba hawajajifunza hata kidogo kutokana na
mashambulizi ya Westgate,” walisema.
Mwezi jana, takribani watu 70 waliuawa baada ya
al-Shabaab kulivamia jengo la Westgate, kituo maarufu cha biashara
kinachotembelewa na matajiri wa Kenya na raia wa kigeni mjini Nairobi.
Watu wengine kadhaa wanaripotiwa kutojulikana walipo
kufuatia shambulizi hilo.
Kundi hilo lilidai kuhusika na tukio hilo. Kiongozi wa al-Shabab,
Ahmed Godane alisema kuwa shambulizi hilo lilikuwa jibu kwa uvamizi wa jeshi la
Kenya kusini mwa Somalia Oktoba 2011.
Kwa sasa Kenya ina zaidi ya askari 4,000 kusini mwa
Somalia, ambapo wamekuwa wakipambana na al-Shabab.
Vikosi vya Kenya ni sehemu ya Kikosi cha Umoja wa Afrika
nchini Somalia (AMISOM) kinachofundishwa na kufadhiliwa na Jumuiya ya
Kimataifa.
Somalia haikuwa na serikali kuu yenye nguvu tangu mwaka
1991, pale wababe wa vita walipomuondoa madarakani kiongozi wa zamani wan chi hiyo
Mohamed Siad Barre.
Hata hivyo, mkutano wa Wabunge uliofanyika Septemba 2012
mjini Mogadishu ulimchagua Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais mpya wa Somalia kwa
kura nyingi.
Serikali ya Somalia imekuwa ikipigana na al-Shabaab kwa
zaidi ya miaka 6 sasa na inaungwa mkono na askari 10,000 wa AMISOM kutoka
Uganda, Burundi, Djibouti na Kenya.
0 comments:
Post a Comment