Papa Francis wa Kanisa Katoliki Duniani amekubali rasmi
ombi la kujiuzulu kwa askofu mmoja wa Ireland aliyekiri kumlinda kasisi mmoja
aliyetuhumiwa kwa udhalilishaji wa watoto.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Vatican leo, William
Lee, Askofu wa Dayosisi ya Waterford na Lismore za Ireland Kusini, aliondolewa
kwenye majukumu yake hayo chini ya Sheria ya Kanisa inayohusisha makosa
makubwa.
Mwaka 2010, Askofu Lee, aliyetawazwa mwaka 1966, alikiri
kwamba majibu yake kuhusu tuhuma za udhalilishaji wa watoto zilizokuwa
zikimkabili kasisi mmoja wa Ireland katikati ya miaka ya 1990 hazikuwa hayakuwa
sahihi, na alifanya hivyo ili kumlinda mtuhumiwa.
Katika miaka ya hivi karibuni, Kanisa Katoliki limekuwa
likilaumiwa kwamba linaficha maovu ya udhalilishaji wa watoto unaofanywa na makasisi
ili kuwalinda na pia kulinda heshima ya kanisa.
Hivi karibuni mimia ya kesi yamefunguliwa huko Ulaya na
Marekani zikiwahusisha watumishi hao.
Matukio ya udhalilishaji wa kingono ndani ya Kanisa
Katoliki yaliibuka katika miaka ya 1980 na kugundulika mwaka 2002 baada ya
mfumo wa kuyafunika kufichuliwa.
Haya yahatokea wakati Papa mpya akikabiliwa na mlima
mkubwa wa tuhuma za udhalilishaji wa kingono zinazoliandama kanisa na kitisho
cha usekula.
0 comments:
Post a Comment