Jaji Mkuu Wa Zanzibar Othman Omar Makungu leo ametoa dhamana
kwa kiongozi mwandamizi Wa Jumuiya Ya Uamsho Sheikh Azzan Khalid Hamdan, Kwa
Ajili Ya Kupatiwa Matibabu Nchini India, Baada Ya Kulazwa Katika Hospitali Ya
Mnazi Mmoja Tangu Septemba Mosi Mwaka Huu.
Jaji Mkuu Wa Zanzibar Ametoa Uamuzi Huo Wa Kumpatia
Sheikh Azzan Dhamana, Baada Ya Kupokea Maombi Kutoka Kwa Mawakili Wa Upande Wa
Utetezi, Wakiongozwa Na Salum Tawfiq.
Tawfiq Ameiomba Mahakama Kuu Ya Zanzibar Impatie Dhamana
Sheikh Azzan, Ili Aweze Kwenda Kutibiwa Nchini India, Kama Ilivyoelezwa Na
Ripoti Ya Madaktari Wa Hospitali Ya Mnazi Mmoja, Ambayo Imekiri Kuwa Maradhi Ya
Kiongozi Huyo Hayatibiki Hapa Nchini Na Hivyo Kutakiwa Kutibiwa Nje Ya Nchi.
Baada Ya Kuwasilisha Maombi Hayo Na Kuambatanisha Na
Ripoti Ya Daktari Pamoja Na Baadhi Ya Nyaraka Nyingine Muhimu, Upande Wa
Mashtaka Umeeleza Kutokuwa Na Pingamizi Dhidi Ya Maombi Hayo Hasa Kwa
Kuzingatia Kuwa Pamoja Na Kuwa Ni Mstakiwa, Ana Haki Ya Kuishi Kwa Mujibu Wa
Katiba.
Katika Uamuzi Wake, Jaji Mkuu Makungu Ametaka Sheikh
Azzan Khalid Hamdan Aachiliwe Kutoka Katika Mikono Ya Askari Wa Magereza Ili
Aweze Kwenda Kutibiwa Nchini India, Ndugu Wawili Wa Kiongozi Huyo Wamchukulie
Dhamana Na Kuhakikisha Anarejea Nchini Mara Baada Ya Kupatiwa Matibabu Pamoja
Na Kuzingatia Ushauri Wa Daktari Utakaotolewa Baada Ya Matibabu Hayo.
Hata Hivyo, Wakili Tawfiq Amesema Safari Pamoja Na
Matibabu Yatagharamiwa Na Familia Ya Sheikh Azzan, Baada Ya Kukamilisha Kwa
Taratibu Zote Za Kisheria.
Sheikh Azzan Pamoja Na Wenzake Tisa Wanakabiliwa Na Kesi
Ya Jinai Namba 9 Ya Uvunjifu Wa Amani Na Uharibifu Wa Mali Za Umma, Ambapo Hadi
Hivi Sasa Viongozi Wako Mahabusu, Baada Ya Mkurugenzi Wa Mashtaka Zanzibar
Ibrahim Mzee Ibrahim Kufunga Dhamana Zao.
0 comments:
Post a Comment