Vikosi vya Ulinzi vya Jeshi la Kenya (KDF) vimeiambia
polisi ya Kimataifa (Interpol) kwamba hawakumuua mwanamke mwenye asili ya
Uingereza anayedaiwa kuratibu shambulio kwenye kituo cha biashara cha Westgate
jijini Nairobi.
Kwa mujibu wa taarifa mpya kutoka Shirika la Habari la
Uingereza (BBC), Samantha Lewthwaite anayejulikana kama “mjane mweupe”
anazunguka kwa uhuru katika mitaa ya Kenya na Interpol wametoa kibali cha
kukamatwa.
Taarifa zinazopingana kutoka kwa Mamlaka za Kenya
zinasema kuwa Samantha hakuwa miongoni mwa wavamizi waliouawa na KDF katika
shambulizi la Jumatatu. Wavamizi watano waliuawa wakati wa mzingiro huo.
Samantha Lewthwaite, amewekwa katika orodha ya watu
wanaosakwa sana na mamlaka za Kenya kwa kupanga shambulizi la kigaidi.
Samantha anadaiwa kuwa mtu hatari sana kwa mujibu wa
shirika la ujasusi la Marekani (CIA) na lile la Israel (Mossad), na anahusika
na vifo vya maafisa wa polisi katika jengo hilo; huko nyuma alifanikiwa
kuikwepa mitego yote ya polisi ndani na nje ya Kenya.
Marekani imetoa kitita cha dola milioni 1 kama zawadi
iwapo atakamatwa akiwa hai au maiti.
CHANZO: Kenyan Daily Post
0 comments:
Post a Comment