NASA WATOA PICHA ZA KISIWA KILICHOIBUKA BAADA YA TETEMEKO LA ARDHI

Photo by NASA


Katika tetemeko kubwa lililotokea nchini Pakistan na kuua zaidi ya watu 500, kisiwa kipya kiliibuka kutoka ndani ya kina cha bahari. Shirika la anga la Marekani, NASA, limetoa picha za kisiwa hicho. 

NASA imetoa picha za kabla na baada ya kutokea kwa kisiawa hicho kilichoibuka Septemba 24 wakati wa tetemeko la ardhi lililoitikisa Pakistan.
 
Kisiwa hicho kinachoitwa Zalzala Jazeera, yaani kisiwa cha tetemeko, kinapatikana umbali wa kilometa 380 kutoka kwenye kiini cha tetemeko hilo ufukwe wa eneo Paddi Zirr jirani na mji wa Swadar, Pakistan katika Bahari ya Arabia.
  
Picha zilizopigwa Aprili 17 zinaonesha kuwa eneo hilo lilikuwa na maji na hapakuwa na ardhi, ilhali picha iliyochukuliwa ilichukuliwa kwa satelaiti Septemba 26 ikionesha kuwa kuna kisiwa kipya.

Photo by NASA
Photo by NASA

Watafiti wa masuala ya Ardhi wanasema kuwa hiki sio kisiwa cha kwanza kutokea umbali wa kilomita 700 kutoka pwani kwa zaidi ya karne moja. wanasayansi wanatabiri kuwa kisiwa hiki kitaendelea kubaki kwa muda wa mwaka mmoja na kisha kitazama tena katika Bahari hiyo ya Arabia.

Kisiwa hicho kiliibuka kutoka baharini wakati wa tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.7 lililopiga katika jimbo la Balochistan, kilometa 69 kaskazini magharibi mwa Pakistan tarehe 24 Septemba 2013. Zaidi ya watu 300,000 waliathiriwa na tetemeko hilo lililosababisha vifo vya watu 500, na kiasi cha nyumba 21,000 kuharibiwa vibaya sana.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment