MKOA wa kusini magharibi wa Fezzan nchini Libya jana
ulijitangaza kuwa jimbo huru na lenye serikali.
Vyombo vya habari nchini Libya vimeripoti kuwa Nouri
Mohammad al-Qouizi alitangazwa kuwa rais wa jimbo hilo. Viongozi wa kikabila
katika eneo hilo wanasema kuwa baadaye watamteua mkuu wa jeshi atakayelinda
mipaka ya jimbo hilo na mali asili zake.
Aidha, viongozi hao wa kikabila wanasema kuwa wamechukua
hatua hiyo kwa sababu ya “utendaji dhaifu wa Baraza Kuu la Kitaifa na
kutoitikiwa kwa matakwa ya watu wa Fezzan.”
Hatua hiyo inakuja mwezi mmoja baada ya eneo la Cyrenai,
mashariki mwa Libya, kuchukua hatua kama hiyo kwa kujitangaza kuwa jimbo huru.
CHANZO: Al-Arabiya
0 comments:
Post a Comment