WFP YAANZA KUGAWA CHAKULA NCHINI MALI

Malian women walk near a refugee camp in Mali’s northwestern city of Dori on December 7, 2012.
Wanawake wa Mali wakitembea jirani na kambi ya wakimbizi katika mji wa Dori kaskazini mwa Mali.
 




SHIRIKA la Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) limeanza kugawa chakula kwa wananchi wa Mali wanaokabiliwa na hali ngumu ya kibinaadamu katika maeneo yaliyokumbwa na vita.


Siku ya Ijumaa, Shirika hilo la Umoja wa Mataifa lilisema kuwa lilifanikiwa kupekeleka misaada ya chakula katika miji ya kaskazini ya Gao na Timbuktu kwa kutumia ndege na boti.


Kwa mujibu wa WFP, idadi ya walengwa inatarajiwa kufikia watu 145,000 katika miji yote miwili.  

Hata hivyo, WFP inasema kuwa bado imekuwa vigumu kutathimini hali ya kibinaadamu katika baadhi ya maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo.


Shirika hilo linasema kuwa takriban asilimia 70 ya familia zinahangaika kupata chakula katika maeneo mengine ya katikati mwa Mali, ikiwemo mji wa Mopti katikati mwa jimbo la Niger Delta.


Ripoti zinasema kuwa barabara za jirani na mji wa Timbuktu zimeendelea kukosa usalama na upungufu wa chakula, na hivyo kuuathiri mji huo baada ya vikosi vinavyoongozwa na Ufaransa kudai kuwa vimewaondoa waasi na kuudhibiti mji huo. 

Takriban wanajeshi 4,000 wa Ufaransa wametumwa nchini Mali tangu Ufaransa ilipoanzisha vita mnamo Januari 11 kwa hoja ya kupambana na waasi waliokuwa wamelidhibiti eneo la kaskazini mwa Mali.



Vita hiyo imesababisha mgogoro mkubwa wa kibinaadamu katika maeneo ya kaskazini mwa Mali na kuwahamisha maelfu ya watu ambao sasa wanaishi katika hali ngumu mno.

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaamini kuwa utajiri mkubwa wa maliasili zinazopatikana nchini Mali, kama vile dhahabu na madini ya urani, inaweza kuwa miongoni mwa sababu za Ufaransa kuanzisha vita hiyo.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment