MRITHI WA CHAVEZ KUPATIKANA APRILI 14

Tibisay Lucena, the president of the CNE, speaks at a press conference at the CNE headquarters in Caracas, on March 9, 2013.
Mwenyekiti wa Tume Uchaguzi ya Venezuela, Tibisay Lucena, akizungumza na vyombo vya habari kwenye makao makuu ya tume hiyo mjini Caracas, jana Machi 9, 2013.




Venezuela itafanya uchaguzi wa rais tarehe 14 Aprili kutafuta mrithi wa marehemu Hugo Chavez.

Tibisay Lucena, mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi ya Venezuela (CNE) alitoa taarifa hiyo kwenye televisheni ya taifa baada ya kukutana na bodi ya wakurugenzi wa tume hiyo mjini Caracas jana Jumamosi.



"Uchaguzi huu utadhamini usalama wa mfumo wa uchaguzi na mchakato mzima...na kudhamini madaraka na mamlaka ya wananchi kwa njia ya kura," alieleza Lucena.

Kampeni za uchaguzi zitaanza Aprili 2 mpaka Aprili 11.


Rais wa muda, Nicolas Maduro atagombea kwa tiketi ya chama tawala. 


Ramon Guillermo Aveledo, Katibu Mtendaji wa Muungano ujulikanao kama Democratic Unity Roundtable, ambao ndio muungano mkuu wa upinzani nchini humo, alitangaza kuwa Henrique Capriles, aliyeshindwa na Chavez katika uchaguzi wa Oktoba 2012, ameteuliwa kugombea kwa mara nyingine dhidi ya Maduro. 

"Tumekubaliana kwa pamoja kumpa ugombea mtu aliyekuwa mgombea wetu katika uchaguzi uliopita," alisema Aveledo. 


Siku ya Ijumaa, Maduro aliapishwa kama rais wa muda baada ya mazishi ya Chavez.


Chavez alizaliwa katika familia maskini mnamo Julai 28, 1954 mjini Sabaneta, katika jimbo la Barinas, Venezuela. 

Alihitimu masomo yake katika Chuo cha Sayansi za kijeshi mwaka 1975.


Chavez alianza kujihusisha na harakati za kimapinduzi akiwa jeshini mwaka 1977.


Mwaka 992, aliongoza jaribio lililoshindwa la kuiangusha serikali ya Rais Carlos Andres Perez na alifungwa kwa muda wa miaka miwili. Licha jaribio hilo kushindwa, tukio hilo lilikuwa mwanzo wa safari yake ya kisiasa.


Chavez alitembea nchi nzima, akiwahamasisha Wavenezuela kwa hotuba zake kali, na alishinda uchaguzi wa rais mwaka 1998. Vile vile alishinda chaguzi za mwaka 2000, 2006, na  2012. 

Mwaka 2002, kundi la wanasiasa na wanajeshi walifanya mapinduzi dhidi ya Chavez. Alikamatwa na kupelekwa katika kambi moja ya jeshi kwenye kisiwa cha Caribbean.


Lakini, siku mbili baadaye, juhudi za wanajeshi watiifu na maandamano makubwa yaliyofanywa na wananchi zimrejesha madarakani.


Chavez alikuwa viungo muhimu katika vuguvugu la maendeleo lililoenea katika nchi zote za Amerika ya Kusini kwa miaka kadhaa.

Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment