Vurugu Kenya, Polisi Wafyatua mabomu ya machozi kwa wafuasi wa odinga



Muandamanaji Akibishana Na Polisi

Maofisa wa polisi wa kenya wamefyatua mabomu ya kutoa machozi kwa mashabiki wa mgombea urais aliyeangukia pua nchini kenya Raila Omolo Odinga.

Shuhuda alisema mashabiki wa Odinga aliyeshindwa na Uhuru kenyatta walikusanyika katika mji wa bandari wa kisumu kwaajili ya kufuatilia matokeo.

Pia walikuwa wakiimba nyimbo “No raila, no peace” wakiwa na maana “hakuna raila, hakuna amani” na kutupia mawe maofisa wa polisi pamoja na gari zilizokatiza.

Mapema leo tume ya uchaguzi nchini kenye ilimtangaza Uhuru Kenyatta kuwa ndie mshindi  wa uchaguzi wa kura za urais.

Hata hivyo waziri  mkuu anayemaliza muda wake na mgombea wa kiti cha urais aliyeshindwa aliwataka wakenya watii utawala wa sheria na kuonya “uvunjifu wa amani wa sasa utalisambalatisha taifa milele”.

Kenyatta, mtoto wa rais wa kwanza wa nchi hiyo Jomo Kenyatta, anakabiliwa na kesi katika mahama ya kimataifa ya jinai kwa kutenda makosa ya kinyume na haki za kibinaadamu yanayohusiana na vurugu za uchaguzi zilizotokea mwaka 2007, na atafika tena Hague july mwaka huu.
Zaidi ya wakenya 100 walikufa na 600,000 waliitoroka nchi yao kufuatia vurugu za 2007 ambapo Odinga alidai Mwai Kibaki alimuiba kura zake

Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment