Wanangangari Mtwara Wamuhitaji Prof Lipumba



BAADHI ya wanachama wa chama cha wananchi CUF wilaya ya Mtwara Vijijini, wameomba viongozi wa kitaifa akiwemo Mwenyekiti wao Profesa Ibrahim Lipumba kufanya ziara za mara kwa mara mikoani.

Wakiongea na Alhuda wilayani humo hivi karibuni, Wanagangari hao wamesema, ni vizuri ziara za viongozi hao wa kitaifa zikahusisha pia maeneo ya vijijini badala ya kuishia wilayani au kwenye makao makuu ya mikoa pekee.

Wamesema, ziara hizo zitasaidia kuimarisha nguvu ya chama, na kuwapa moyo wanachama waliokata tamaa.
Mjumbe wa chama hicho Mtwara vijijini Jamar Said amesema, uhai wa chama unategemea ukaribu wa viongozi wa ngazi zote kuanzia matawini hadi taifa na wanachama wao.

“Wanachama wapo, lakini tatizo kubwa ni kukosekana kwa hamasa toka kwa viongozi, na hasa wa kitaifa hususan katika maeneo ya vijijini”, akasema mwanasiasa huyo.
Amewashauri viongozi wa taifa wa chama hicho kujipanga kupanga namna bora ya kuwafikia wananchama hasa maeneo ya vijijini, kwa minajili ya kuimarisha chama.

Naye mwanachama wa chama hicho Bwana Rashid Nandonde, amesema, Mtwara ni ngome muhimu ya chama, hicho ni vema ikaimarishwa.

“Unajua ngome mojawapo muhimu ya CUF ipo katika Mikoa ya kusini, hivyo kuwaacha wanachama muda mrefu bila kuwatembelea ni kupoteza nguvu ya chama” akaeleza mwanachama huo. Bibi Siwajibu Khalfan mwanachama mwingine wa CUF wilayani humo, amesema wakaazi wa vijijini wamechoshwa na hali ya mambo inavyoendeshwa na chama twala, hivyo ni vema fursa hiyo ikatumika vizuri na viongozi wao kuanzia ngazi ya tawi hadi taifa kupanua wigo wa wanachama wao vijijini.

Mbali na kuwahitaji viongozi kuwatembelea, wanachama hao pia wamehamasichana juu ya umuhimu wa kufungua matawi ya chama hicho.

”Hili tumekuwa tukiwakumbusha viongozi wetu wa ngazi zote mara kwa mara. Chama bila matawi si chama” anaeleza Bibi Mwajuma Suleiman.

Aidha wametoa angalizo kwa viongozi wao wa kitaifa kuwa makini ili ngome zao mikoani zisiangukie katika mikono ya vyama vingine.

Wamesisitiza kuwa, Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma (hasa wilaya ya Tunduru) ni ngome imara na muhimu za CUF, hivyo ni vema chama kikajipanga vizuri kuzihifadhi.

chanzo:al-huda

Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment