Kamati kushughulikia mgogoro wa uchinjaji yaundwa

SERIKALI nkoani Mwanza imeunda kamati ya pamoja ya madhehebu ya Kikristo na Kiislamu kushughulikia mgogoro  wa uchinjaji ulioibuka hivi karibuni katika maeneo ya Kanda ya Ziwa.

Kuundwa kwa kamati hiyo yenye wajumbe 20 kutoka madhehebu yote mawili kutokana na agizo la Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alilotoa Februari 16 mwaka huu alipokuwa mkoani hapa kutafuta ufumbuzi wa mgogooro huo.

Ziara ya Pinda ilitokana na vurugu na mauaji katika mji mdogo wa Buseresere mkoani Geita.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo alisema kamati hiyo imekutana na kushauriana na kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Mwanza.

Ndikilo alisema baada ya kuzinduliwa kamati hiyo iliwachagua viongozi wake ambao wataunda kamati ya ndogo ya watu wanne Mwenyekiti akiwa Sheikh Hassan Kabeke na Makamu wake Askofu Charles Sekelo.

Katibu ni Askofu Zenobius Isaya wakati Msaidizi wake ni Sheikh Mohamed Bara.

Alisema kikao hicho kilitoa maazimio matano likiwamo kuundwa kwa kamati hiyo ndogo ya viongozi wanne itakayoratibu na kuangalia mambo muhimu yatakayoshughulikiwa na kujadiliwa kabla ya kufikishwa kwenye kamati ya wajumbe wote. 

Kamati ya wajumbe wote itayajadili kwa umakini kabla ya kupeleka mapendekezo kwa kamati ya Serikali ili yajadiliwe na kutolewa uamuzi.

Maazimio mengine ni kupitia viashiria vyote vinavyolenga vurugu na uvunjifu wa amani katika Mkoa wa Mwanza, kuviainisha na kuviandaa kwa kuvifanyia tathimini na kamati kukutana kila mwezi mara moja kubadilishana mawazo. 

Ndikilo alisema kamati hiyo pia imekubaliana kuanzishwa kamati za wilaya kwa utaratibu huo wa kamati ya mkoa lengo likiwa ni kumaliza tofauti zinazokuwa zimejitokeza.

CHANZO: MTANZANIA
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment