Makao Makuu Ya Chama Cha Mpira Wa Miguu Misri Yachomwa Moto




Mashabiki  wa soka nchini misri wamechoma moto  makao makuu ya chama cha mpira wa miguu nchini hapo pamoja na ukumbi wa klabu ya polisi uliopo mjini cairo baada ya hukumu ya mahakama kuhusu maandamano yaliyosababisha vifo mwaka jana.
msemaji wa polisi alisema mashabiki wenye hamasa walivamia ukumbi wa klabu ya polisi na kuvunja majengo kadhaa jumamosi.
Ripoti hiyo inaeleza baadhi ya majengo yaliachwa yakiwa hayana milango.
Katika hali inayofanana waandamanaji walivamia pia makao makuu ya chama cha mpira na kuichoma hasa.
Vurugu hizo zilizuka saa kadhaa baada ya mahakama ya kesi za jinai kutoa hukumu ya vifo kwa watuhumiwa 21 waliohusika na maandamano ya vurugu yaliyofanyika mwaka 2012 Port Said kwasababu  za kimichezo. Mahakama hiyo iliwahukumu watuhumiwa 5 kifungo cha maisha, 19 jela  kwa muda mfupi na kuwaachia huru wengine 28.
Wapambanaji hao waliawasha moto ambao ulisambaa mpaka nyumba za karibu na jengo hilo.
Runinga ya taifa ya nchi hiyo imeripoti kuwa mamia ya wamashabiki wa mpira wa miguu wapo njiani kuelekea wizara ya mambo ya ndani.
Tangia march 3 , zaidi ya watu 7 imeripotiwa kuawa na maelfu kuumia katika jiji la Suez Canal liliopo Port Said, mauaji haya ni muendelezo wa vurugu kama hizo zilizotokea kuanzia january mwaka huu.
Waandamanaji hao wanasema wamepandwa na hamasa kwasababu ndugu zao wa mji mmoja ndio amabao amekutwa na hatia ya kuua watu 74, kutokana na maandamano yaliyotokea katika mji huo baada ya timu ya mji huo Al-Masry kuifunga Al-Ahly ya mji wa Cairo kwa magori  3-1 katika mechi ya mpira wa miguu iliyochezwa mwaka jana.
January, jaji alihukumu  kunyongwa watu 21 kwa kuhusika kwao katika vurugu za  february 1, 2012 ambazo zilipelekea watu 1,000 kuumia.
Misri inapinga vurungu hizo  na kueleza kwamba vurugu hizo zinaendeshwa na kisiasa



Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment