SIKU AMBAYO PAPA ALIMUINAMIA MUGABE KWA HESHIMA


Papa Francis ameibua utata katika siku yake ya kwanza kazini baada ya kukutana na kusalimiana na Rais wa Zimbazwe, Robert Mugabe, wakati wa kutawazwa kwake mjini Vatican jana.

Rais Mugabe, ambaye amewekewa vikwazo vya kusafiri kutoka Jumuiya ya Umoja wa Ulaya tangu mwake 2002 kutokana na tuhuma za kukiuka haki za binaadamu na wizi wa kura, alikuwa amekaa sehemu ya watu maalumu (VIP) katika Medani ya St. Peter wakati wa sherehe za kusimikwa kwa papa mpya na baadaye alisalimiana na kuongea na papa huyo.

Maafisa wa Vatican walijaribu kupuuza marufuku hiyo iliyowekwa dhidi ya Rais Mugabe mwenye umri wa miaka 89, wakidai kuwa waumini wote wa Kikatoliki walialikwa kwenye sherehe hizo na kwamba hakuna mwaliko binafsi uliotolewa kwa rais huyo kabla ya sherehe.

Rais Mugabe amewekewa vikwazo kutotembelea nchi za Jumuiya ya Umoja wa Ulaya, lakini Vatican sio mwanachama wa Umoja huo.





Respecting Mugabe: Pope Francis bows his head for the 89-year-old Zimbabwean despot as they meet at St Peter's Basilica during the inaugural Mass
Heshima kwa Mugabe: Papa Francis akiiniamisha kichwa chake kuonesha heshima kwa Rais Mugabe.


Well received: The new pontiff smiles as he chats to President Mugabe and his wife, who were greeted at the airport by a priest sent specifically to welcome them to the Vatican
Rais Robert Mugabe na mkewe, wakizungumza na papa mpya


Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment