MILIPUKO YA MABOMU YAITIKISA UTURUKI



Police officers stand at the site of an attack on the Turkish Justice Ministry in Ankara on March 19, 2013.
Maofisa wa Polisi wakiwa eneo la tukio kwenye jengo la Wizara ya Sheria mjini Ankara, Machi 19, 2013



Shambulizi la bomu limepiga kwenye Wizara ya Sheria nchini Uturuki, na milipuko mingine miwili imepiga kwenye makao makuu ya Chama Tawala cha Haki na Maendeleo (AKP) na makao makuu ya Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Mawasiliano nchini humo.

Kwa mujibu wa gazeti la Zaman la nchini humo, jana jumanne, mshambuliaji asiyejulikana alitupa mabomu mawili madogo kwenye jingo la Wizara ya Sheria, na kundi la watu wenye silaha likayshambulia makao makuu ya chama tawala kwa kutumia silaha nyepesi inayotumika kukabiliana na kifaru.

Watu wawili walijeruhiwa katika mlipuko wa bomu uliotokea kwenye jengo la Wizara ya Sheria.

Ripoti zinasema kuwa Polisi wamewakamata watu wawili wanaoshukiwa kuhusika na shambulio lililotokea kwenye wizara hiyo.

Hata hivyo, Waziri wa mambo ya ndani, Muammer Guler alikanusha taarifa za vyombo vya habari, akisema kuwa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na shambulio hilo.

Katika taarifa yake, Waziri wa Sheria, Sadullah Ergin alilaani vikali hujuma hizo.

Wakati huo huo, hakuna maafa yaliyotokea katika shambulio lililoyalenga makao makuu ya chama cha AKP, ambalo lilisababisha tu uharibifu wa mali na vifaa katika jingo hilo.

Mapema siku hiyo, watu wanne walijeruhiwa katika mlipuko mwingine wa bomu uliotokea kwenye makao makuu ya Chama cha Wafanyakazi wa sekta ya Mawasiliano mjini Ankara.

Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment