RAIS WA AFGHANISTAN HAMID KARZAI ASEMA: TALEBAN NA MAREKANI WANAFANYA MAZUNGUMZO KILA SIKU

Afghan President Hamid Karzai
Rais wa Afghanistan, Hamid Karzai




Rais wa Afghanistan Hamid Karzai amefichua kuwa kundi la wanamgambo wa Taliban na Marekani wamekuwa wakifanya mazungumzo kila siku nchini Qatar.


“Viongozi waandamizi wa Taliban na Wamarekani wanafanya mazungumzo kila siku katika taifa hilo la Ghaba," Karzai aliuambia umati wa watu uliokusanyika kuadhimisha siku ya  Wanawake Duniani.


Hata hivyo, msemaji wa Taliban, Zabihullah Mujahid, alisema kuwa kundi lake "linakanusha maelezo ya Karzai." Mujahid aliongeza kuwa hakuna maendeleo yaliyopatika katika mazungumzo hayo tangu yalipositishwa mwaka mmoja uliopita.


Mwezi uliopita, vyombo vya habari za Afghanistan viliripoti kuwa Washington ilikuwa ikifanya mazungumzo na Taliban nchini Qatar ili kulishawishi kukaa kwenye meza ya mazungumzo pamoja na serikali ya Afghanistan.


Maafisa wa serikali ya Afghanistan hawajafanya mazungumzo ya ana kwa ana na wanamgambo hao tangu walipoangushwa mwaka 2001.


Taliban imekuwa ikikataa kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na serikali ya Karzai inayoungwa mkono na nchi za Magharibi, wakitaka mazungumzo yafanyike kati ya kundi hilo na Marekani.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment