RAIS OBAMA AWASILI ISRAEL

US President Barack Obama sits next to Israeli Prime Minister Benjamin Netanyahu during a welcome ceremony at Ben Gurion International Airport near Tel Aviv, on March 20, 2013.
Rais Barack Obama na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu wakati wa sherehe ya makaribisho kwenye Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion.




Rais wa Marekani, Barack Obama amewasili mjini Tel Aviv kama sehemu ya ziara yake katika eneo la Mashariki ya Kati, huku maandamano dhidi ya ziara yake hiyo yakishtadi katika eneo la Ukanda wa Magharibi.


Rais Obama alikaribishwa na Rais wa Israeli Shimon Peres, na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ben Gurion  jirani na Tel Aviv.


Baada ya kuwasili, Obama alirejea ahadi ya nchi yake kuendelea kuinga mkono Israeli.


Ripoti zinasema kuwa katika ziara hiyo hakuna ahueni inayotarajiwa katika mazungumzo ya amani baina ya Waisraeli na Wapalestina.


Wapalestina wamefanya maandamano dhidi ya mpango wa Obama wa kulitembelea eneo la Ukanda wa Magharibi linalokaliwa kwa mabavu, wakisema kuwa Obama hafanyi vya kutosha kuzuia shughuli za Israeli za ujenzi wa makazi ya walowezi na ukamataji holela wa Wapalestina unaofanywa na vikosi vya Israeli.


Mwezi Desemba 2012, maafisa wa Israeli walisema kuwa wataendelea na mipango ya kujenga makazi zaidi ya walowezi katika maeneo ya Wapalestina, licha ya upinzani wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Kimataifa dhidi ya hatua hiyo.



Upanuzi wa makazi ya walowezi wa Kiyahudi unaofanywa na Israeli katika ardhi ya Palestina umetengeneza kikwazo kikubwa dhidi ya juhudi za kuleta amani Mashariki ya Kati.


Zaidi ya Waisraeli milioni moja na nusa wanaishi katika zaidi ya makazi haramu ya kilowezi 120 yaliyojengwa na tangu Israeli ilipoyakalia kimabavu maeneo ya Wapalestina ya Ukanda wa Magharibi na Mashariki mwa Jerusalemu mwaka 967. 

Umoja wa Mataifa na nchi nyingi zinayaona makazi hayo ya kilowezi kuwa makazi haramu kwa sababu maeneo hayo yalitwaliwa kwa mabavu na Israeli katika vita ya mwaka 1967 na hivyo yanahusika na Mkataba wa Geneva, ambao unapiga marufuku kujenga katika ardhi zilizotwaliwa kimabavu.

Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment