RAIS WA BANGLADESH AFARIKI DUNIA

Aliyekuwa Rais wa Bangladesh, Zillur Rahman



Rais wa Bangladesh, Zillur Rahman amefariki dunia katika hospitali nchini Singapore akiwa na umri wa miaka 84 baada ya maradhi yaliyomsumbua kwa muda mrefu.


Zillur Rahman alipelekwa Hospitali ya Mount Elizabeth nchini Singapore tarehe 10 Machi kwa matibabu ya matatizo ya kushindwa kupumua vizuri.


Kifo cha mwanasiasa huyo mkongwe kutoka chama tawala hakitaiathiri serikali kwa sababu Bangladeshi ni nchi inayofuata mfumo wa Demokrasia ya Kibunge, ambapo Waziri Mkuu ndiye mwenye mamlaka ya kiutendaji.


Ofisi ya Rais imesema kuwa spika wa bunge Abdul Hamid atakaimu kama rais wa nchi mpaka bunge litakapomteua mtu mwingine.


"Kaimu rais ametangaza siku tatu za maombolezo kwa kifo cha Rais Zillur Rahman," alisema  msemaji wa rais kama alivyonukuliwa na shirika la habari la serikali, Bangladesh Sangbad Sangstha.


Zillur Rahman aliwahi kuwa naibu mkuu wa chama tawala cha Bangladesh cha Awami, kabla ya kuchaguliwa na bunge kuwa rais mwaka 2009.


Katika salamu zake za rambirambi, Waziri Mkuu, Sheikh Hasina alimuelezea Rahman kama kiongozi mzalendo.


Zillur Rahman ameacha watoto watatu, mmoja akiwa ni wa kiume na ambaye pia ni mwanasiasa, na mabinti wawili.

Mke wa Zillur Rahman, Ivy, ambaye pia alikuwa mwanasiasa, alifariki mwezi Agosti 2004 baada ya kujeruhiwa vibaya katika shambulizi ya bomu la kutupwa kwa mkono lililofanywa dhidi ya maandamano ya Chama cha Awami na kuua watu wengine 20.

CHANZO: ALJAZEERAH
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment