Kesi Ya Sheikh Ponda Imezidi Kufichua Makubwa

Mzee Waikela (Aliyeshikiliwa) Akitoka Kutoa Ushahidi Mahakama Ya Kisutu
Katika muendelezo wa ushahidi wa utetezi katika kesi inayomkabili Sheikh Issa Ponda na waislamu wenzake 49 ,mwanzilishi wa Baraza la Misikiti Tanganyika, Mzee Bilali Waikela (87),amesema   "Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais wa kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Aman Karume,ndio waliovunja Umoja wa Waislamu wa Afrika Mashiriki, umoja huo ulianzishwa kwa lengo la kuwatetea na kuwasaidia Waislamu, na pia kiwanja cha Markaz Chang'ombe kilipatikana kutoka kwa aliyekuwa Rais wa Misri Jamal Abdul Naser na kuwagawia waislamu wa Tanzania"
 
 
“Mwalimu Nyerere ndiye aliyemtuma Karume kuvunja umoja huo na mimi mwaka 1964 nilifungwa baada ya kukataa kupokea Shilingi 40,000 ili nikubali kuvunja umoja wetu, na  Kassim bin Juma, Adam Simba na Salehe Masasi ndio waliotumiwa kuhamasisha watu kuvunja umoja huo” aliongeza Mzee Waikela. 
 
Mzee Waikela ambaye ni mwenyeji na mkazi wa Tabora aliendelea kusema, ofisi za East Africa Muslim Welfare Society(EAMWS)  zilifungwa mwaka 1968 na ndipo lilipoundwa Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) na kukabidhiwa ofisi pamoja na mali zote kikiwamo kiwanja cha Chang’ombe markaz kilichokuwa kimejengwa shule ya Waislamu.

 
Mzee Waikela ambaye ni shahidi wa 48 wa upande wa utetezi katika kesi hiyo aliendelea kusema 
"umoja huo ulifutwa baada ya Karume kudanganywa kuwa kuna watu wana mpango wa kufanya mapinduzi na kuwarudisha Waarabu Zanzibar"
 

 

Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment