Korea Kaskazini imefanya majaribio 6 ya silaha za
nyuklia – likiwemo jaribio la Jumapili ya leo. Jaribio la kwanza lilitokea
zaidi ya muongo mmoja uliopita katika harakati za taifa hilo kuwa miongoni mwa
mataifa machache yanayomiliki silaha za nyuklia.
Oktoba
2006 - Pyongyang ilifanya jaribio lake la kwanza la silaha za
nyuklia katika handaki moja katika eneo la Punggye-ri lenye milima mingi
kaskazini mwa nchi hiyo.
Jaribio hilo lilisababisha mlipuko wa kilotani (kilotani
moja = tani 1,000) hatua ambayo ililaaniwa na jumuiya ya kimataifa.
Baada ya jaribio hilo, Wakala wa Jiolojia nchini
Marekani (USGS) ilisema kuwa ilibaini tetemeko la lenye uzito wa kiwango cha 4.2
kwenye Rasi ya Korea.
Mei
2009 - Pyongyang ilifanya jaribio lake la pili. Mlipuko wake,
kama ilivyokuwa kwa jaribio la mwaka 2006, ulifanyika chini ya ardhi. Wakala wa
Jiolojia nchini Marekani ilisema kuwa jaribio la bomu hilo lilisababisha
tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 4.7 katika eneo la Kilju kaskazini mashariki
mwa nchi hiyo.
Mlipuko huo ulikuwa na uzito unaokadiriwa kuwa kilotani 2-8.
Mlipuko huo ulisikika katika mji wa Yanji nchini China ambao uko mpakani kwenye
umbali wa kilometa 200.
Februari
2013 – Nchi hiyo ilifanya jaribio la tatu na la kwanza chini
ya utawala mpya wa Kim Jong-un. Jaribio hilo lilikuwa kubwa zaidi ya majaribio
mawili ya mwanzo ambapo wataalamu walikadiria kuwa bomu hilo lilikuwa na uzito
wa kilotani sita mpaka saba.
Pyongyang ilisema kuwa ilitumia “kifaa cha nyuklia
kilichopunguzwa nguvu lakini chenye nguvu ya mlipuko mkubwa zaidi ya milipuko
ya mwanzo”.
Wataalamu nchini Japan, Korea Kusini na Marekani
walisema kuwa tetemeko katika eneo la Punggye-ri likuwa na nguvu kati ya 4.7 na
5.2.
Januari
2016
– Korea Kaskazini ilisema kuwa ilifanya jaribio la nne la bomu la hydrogen.
Tetemeko la ukubwa wa 5.1 lilibainika takriban kilometa 50 kutoka mji wa Kilju,
jirani na eneo la Punggye-ri ambalo kuna vinu vya nyuklia.
Wataalamu walikadiria kuwa bomu hilo lilikuwa na uzito
wa kati ya kilotani nne na sita.
Septemba 2016 – Tetemeko lenye ukubwa wa 5.3 lilitokea
baada ya mlipuko wa takribani kilotani 10 – mara 10 zaidi ya jaribio la kwanza
lililofanywa na Pyongyang muongo mmoja uliopita.
Tetemeko hilo, kama lile la miezi tisa kabla,
lilibainika karibu na eneo la majaribio ya nyuklia kwenye mahandaki ya Punggye-ri.
Septemba
2017 – Tetemeko la ukubwa wa 6.3 labainika katika eneo la Kilju,
mahala linapopatikana eneo la majaribio ya nyuklia la Punggye-ri. Jaribio hilo
jipya ndio jaribio kubwa kabisa kufanywa na Korea Kaskazini mpaka sasa.
Jaribio hilo ambalo ni la kwanza tangu Rais Donald Trump
aingie madarakani, linakadiriwa kuwa na uzito wa mpaka kilotani 100 – karibu mara
nne mpaka tano ya bomu ambalo Marekani ililidondosha kwenye mji wa Nagasaki
nchini Japan.
0 comments:
Post a Comment