Raia wa Rwanda leo wanaelekea kwenye masanduku ya kupigia
kura kumchagua rais wa nchi hiyo. Watu wanaokadiriwa kuwa milioni 6.9
wanatarajiwa kushiriki katika zoezi hilo ambalo lilianza jana kwa kupiga kura
wanyarwanda wanaoishi nje ya nchi.
Vituo 2,340 vimesambazwa kote nchini Rwanda na
vilitarajiwa kufunguliwa mapema leo saa moja kamili asubuhi kwa majira ya Rwanda.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Rwanda,
Charles Munyaneza amesema anatarajia uchaguzi wa leo utafanyika kwa amani na
utulivu kutokana na maandalizi mazuri yaliyofanyika. Munyaneza amesisitiza
kuwa, matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu wa leo nchini Rwanda yataanza kutolewa
leo usiku.
Paul Kagame |
Wagombea watatu wanachuana katika uchaguzi wa leo na
inatabiriwa kwamba rais wa sasa wa nchi hiyo Paul Kagame atapata ushindi
mkubwa.
Wagombea wengine ni Frank Habineza, wa chama cha
Democratic Green Party of Rwanda na Bwana Philippe Mpayimana anayegombea kama
mgombea huru.
Waangalizi 2000 kutoka nje ya nchi wanasimamia uchaguzi
wa leo nchini Rwanda ambao utagharimu Franga za Rwanda bilioni 6.2.
Mgombea wa Chama cha Upinzani cha Democratic Green Party Frank Habineza. |
Uchaguzi wa leo nchini Rwanda unafanyika kwa amani ingwa
ofisi ya shirika la Amnesty International katika kanda ya Afrika mashariki
imetahadharisha kwamba huwenda ukafanyika katika anga ya hofu inayotokana na
ukandamizaji wa miaka mingi wa serikali dhidi ya kambi ya upinzani.
0 comments:
Post a Comment