Leo ni Jumatatu tarehe 10 Julai, 2017.
Miaka 276 iliyopita ardhi ya Alaska iligunduliwa na
mvumbuzi wa Kidenmark, Vitus Bering.
Mvumbuzi huyo aligundua ardhi ya Alaska inayopatikana kaskazini magharibi mwa
Canada akiwa katika safari yake kuelekea Urusi. Hadi kufikia mwaka 1867 eneo
tajiri kwa mafuta la Alaska lilikuwa sehemu ya mamlaka ya Urusi ya Kitezari.
Hata hivyo mwaka huo Urusi iliiuzia Marekani ardhi ya Alaska kwa kiasi cha dola
milioni saba, eneo ambalo leo hii linahesabiwa kuwa jimbo la 49 la Marekani.
Vitus Bering |
Siku kama ya leo miaka 77 iliyopita inayosadifiana na 10
Julai 1940 Jemedari Henri Petain Waziri Mkuu wa muda na afisa wa ngazi ya juu
wa jeshi la Ufaransa, alichukua uongozi baada ya Ufaransa kushindwa na Wanazi
wa Ujerumani katika Vita vya Pili vya Dunia. Kwa mujibu wa mkataba wa kivita
uliosainiwa na nchi mbili hizo tarehe 22 Juni 1940, eneo la kaskazini mwa
Ufaransa, ukiwemo mji wa Paris lilibaki chini ya himaya ya jeshi la Manazi wa
Ujerumani.
Jemedari Henri Petain |
Miaka 44 iliyopita katika siku kama ya leo, visiwa vya
Bahamas huko Amerika ya Kati vilipata uhuru kutoka Uingereza na siku kama ya
leo hufahamika visiwani humo kama siku ya taifa. Visiwa vya Bahamas
viligunduliwa mwaka 1492 na mvumbuzi wa Ulaya Christopher Columbus na kuwa
chini ya himaya ya Uhispania. Visiwa vya Bahamas vilipata uhuru mwaka 1973 na
kuwa mwanachama wa Umoja wa Mataifa. Visiwa vya Bahamas viko kaskazini mwa Cuba
na kusini mashariki mwa Marekani.
Bendera ya visiwa vya Bahama |
0 comments:
Post a Comment