Hii ni picha ya kwanza ya mabaki ya ndege iliyoanguka katikati wa nchi ya Colombia Novemba 28, 2016. |
Ndege iliyobeba watu 81, wakiwemo wachezaji wa soka
kutoka Brazil, imeanguka nchini Colombia, huku maafisi wakisema kuwa kuna
manusura sita.
Ndege hiyo, ikiwa imebaba wachezaji wa timu ya soka ya Chapecoense Real kutoka Brazil ambao ni
sehemu ya abiri 72 na wafanyakazi 9, imeanguka leo jirani na mji wa Medellin
nchini Colombia.
Mamlaka nchini humo
zinasema kuwa waokoaji walikuwa wakiwaondosha manusura kutoka eneo la ajali. Uongozi
wa uwanja wa ndege wa Medellin unasema kuwa eneo hilo lingeweza kufikiwa kwa
barabara tu kwa sababu ya hali mbaya ya hewa.
Ndege hiyo imeanguka
katika eneo liitwalo Cerro Gordo, takriban kilometa 50 kutoka Medellin,
ambao ni mji wa pili kwa ukubwa nchini Colombia.
“Inaonekana kuwa ndege
hiyo iliishiwa mafuta,” Elkin Ospina, meya wa mji wa jirani wa La Ceja,
ameliambia shirika la habari la AFP.
Timu hiyo ya mpira ilikuwa
ikitarajiwa kushiriki katika mchezo wa Kombe la Amerika Kusini katika mji wa
Medellin siku ya Jumatano.
0 comments:
Post a Comment