
Kiungo wa zamani kutoka nchini Brazil, Ronaldinho,
amesema kuwa mchezaji nyota wa Barcelona, Lionel Messi bado ni mchezaji bora
duniani licha ya kutofainikiwa kushinda kombe katika michuano ya kimataifa
akiwa na timu ya taifa ya Argentina.
Messi mwenye umri wa miaka 29 alijiuzulu katika timu
yake ya taifa mapema mwezi huu baada ya Argentina kushindwa kunyakua kombe la
michuano ya Copa America dhidi ya Chile iliyofanyika nchini Marekani.
Mshindi huyo wa mara tano wa Ballon d’Or, aliisaidia
timu yake ya taifa kufika fainali nne ikiwemo ile ya Kombe la Dunia la mwaka
2014 dhidi ya Ujerumani, lakini mar azote hakufanikiwa kunyakua kombe licha ya
kwamba ndiye mfungaji anayeongoza katika timu ya taifa ya Argentina akiwa na
magoli 55 katika michezo 113.
Hivi karibuni nyota wa klabu ya Real Madrid, Cristiano
Ronaldo, aliisaidia Ureno kutwaa taji la michuano ya Mataifa ya Ulaya
iliyofanyika nchini Ufaransa na kuibua mjadala wa nani hasa ni mchezaji bora wa
dunia kwa sasa, lakini Ronaldinho anamuunga mkono mchezaji mwenzake wa zamani
kutoka Barca.
Ronaldinho anasema: “Kwangu mimi, Messi kuacha kushiriki
timu ya taifa haibadilishi chochote. Bado anaendelea kuwa mchezaji bora wa
dunia. Heshima niliyonayo kwake haijabadilika hata kidogo.
“Na kama kweli ameamua kuacha kushiriki soka la
kimataifa basi mchezo huo utamkumbuka, na hata mashabiki zake.”
WhatsApp: +255 712 566 595
0 comments:
Post a Comment