![]() |
| Arsene Wenger Kocha wa Arsenal |
Arsene Wenger amesema kuwa Gary Neville hakuwa sahihi
kudai kwamba meneja huyo wa Arsenal “hajui au ni mwenye kiburi” kwa kutokifanyia
marekebisho kikosi chake kuendana na washindani wake wa Ligi Kuu.
Kabla ya sare tasa na Liverpool jana Jumatatu, Neville alisema
kwenye kipindi cha televisheni kuwa Arsenal ilihitaji kusajili wachezaji wapya
wenye “uwezo” ili kuwapa nguvu zaidi wachezaji wenye vipaji Washika bunduki
hao, na kusema kuwa kiburi pekee ndicho kinachomfanya Wenger asitumie mbinu
mpya.
Alipoulizwa kuhusu kauli za Neville baada ya mchezo huo,
Wenger alisema: "Kila mtu ana mawazo yake. Ninaweza kukuthibitishia kuwa
hilo sio lazima liwe sahihi.”
Neville alikuwa akizungumzia tabu anayoipata Francis
Coquelin na Santi Cazorla wanapocheza nafasi ya kiungo kabla ya kufanya mabadiliko
hafifu ya Calum Chambers na Gabriel.
"Kwangu mimi ni kiburi. Naamini ni kiburi. Hivyo ndivyo
ninavyoamini,” alisema Neville. Kudhani kwamba hutaifanyia marekebisho timu
yako kuendana na nguvu za timu unazocheza nazo.
"Ama hajui, au ni kiburi. Kwa sababu wanaendelea
kupoteza michezo namna hii. Nadhani ni kosa.
"Nina heshima kubwa kwa Arsenal kama klabu. Kazi ya
Arsene Wenger ni nzuri sana.
"Lakini sioni kwa nini hasajili wachezaji wapya
kusaidiana na wachezaji hawa wenye vipaji ulio nao ili kuwawezesha kushinda
ligi.
"Ni tatizo kubwa kwa Arsene Wenger kwa miaka hii 10
ukiangalia kwa nini hajagundua tatizo kwa aina hii ya wachezaji [kama vile Coquelin
na Cazorla] – kwa sababu hawawezi kushinda ligi wakiwa nao. Haiwezi kutokea.
"Sina neno muafaka linaloweza kuwaelezea. Ninaweza kufanya
hivyo, lakini haitakuwa na manufaa kulizungumza kwenye televisheni.
"Wao si wachezaji wanaweza kukufanya ushinde ligi…
unahitaji wachezaji imara, wenye nguvu unazozihitaji kwenye timu kuweza kukabiliana
na timu nyingine ikiwa Blackburn au Manchester
City yenye wachezaji imara kama Yaya Toure na Vincent Kompany."
Wenger aliyakosoa vikali matamshi hayo baada ya timu
yake kuweza kutoa sare ya kutofungana na Liverpool.
"Utapata aina zote za sifa kwangu tangu nilipofika
hapa,” Wenger alisema. “Nimefanya kazi yangu vizuri kwa miaka 20. Ninawaachia wengine
watoe tathmini ya kiwango cha kazi yangu.
"Unapokuwa hujashinda unachukuliwa vibaya na watu
hupata sababu za kusema. Je, ni sababu nzuri? Nina uzoefu wa kutosha kujua ni
wakati gani muafaka na upi ambao sio muafaka.

0 comments:
Post a Comment