![]() |
| Rais Mahmoud Abbas wa Palestina |
Rais wa Palestina Mahmoud Abbas amejiuzulu wadhifa wake
wa mkuu wa kamati kuu ya Chama cha Ukombozi wa Palestina (PLO).
Zaidi ya nusu ya wajumbe wa kamati hiyo yenye wajumbe 18
nao pia wamejiuzulu. Shirika la habari la AFP limemnukuu afisa wa PLO, Wassel
Abu Yussef, akithibitisha hilo bila kutoa maelezo ya ziada.
Yussef ameongeza kuwa Baraza la KItaifa la Palestona
limepanga kukutana ndani ya kipindi cha mwezi mmoja kuteua kamati kuu mpya.

0 comments:
Post a Comment