![]() |
Eneo la mlipuko lililoua watu wasiopungua 20 katika mji
wa Maiduguri, kaskazini mashariki mwa Nigeria, Juni 22, 2015.
|
Milipuko miwili ya mabomu katika eneo la soko na kizuizi
cha jeshi katika eneo la kaskazini mashariki ya Nigeria imewaua watu kadhaa.
Mlipuko wa kwanza umetokea katika soko lenye msongamano
katika kijiji cha Malari, nje ya mji wa Maiduguri. Kwa uchache watu 10
wamepoteza maisha katika mlipuko huo.
Dakika kadhaa baadaye, gari aina ya taksi lililipulika
katika kizuizi kimoja cha jeshi na kuwaua abiria wawili na afisa usalama mmoja.
Mpaka sasa hakuna kundi lililodai kuhusika na
mashambulizi hayo huku ghasia zikigharimu maisha ya zaidi ya watu 160 ndani ya
wiki moja nchini humo.
![]() |
Lango kuu la soko mjini Maiduguri lililofungwa Machi 7,
2015 baada ya mlipuko wa bomu.
|
Katika mashambulizi hayo mabaya, wanamgambo wanadaima
kuilenga misikiti kadha katika mji wa kaskazini mashariki wa Kukawa mnamo Juni
30 na kuwaua waumini wapatao 100.
Wanamgambo hao wameongeza mashambulizi yao tangu Rais Muhammadu
Buhari alipoingia madarakani mwishoni mwa mwezi Mei.
Rais Buhari, ambaye ni jenerali mstaafu, ameapa
kupambana na kundi la Boko Haram na kuliteketeza kabisa.
Uasi wa kundi hilo ulianza mwaka 2009 na umesababisha
vifo vya watu wapatao 15,000 ndani ya miaka sita.


0 comments:
Post a Comment