Pikipiki Yachomwa Moto kwa Kukwapua Simu ya Mtu

 Ule usemi wa za mwizi ni arobani,umetimia leo baada ya vijana wawili wanaotumia pikipiki (majina yao hayakupatikana mara moja) wenye utaalamu wa hali ya juu wa kukwapua simu za mikonini za watu wawapo kwenye magari au hata watembea kwa miguu kushindwa kufurukuta mbele ya wananchi wenye hasira.Tukio hilo limetokea jioni hii mbele ya bustani ya Botanical kwa upande unaotazamana na geti kuu la kuingia Hospitali ya Ocean Road,baada ya kumkwapulia simu mwanadada mmoja (jina kapuni) aliekuwa akitembea kwa miguu na kwa bahati nzuri kulitokea msamalia aliekuwa na gari yake akaliona tukio zina na hapo ndipo alianza kuwafukuzia na mwisho wa mbio hizo ndio ukafika hapa baada ya kuzidiwa maarifa na pikipiki yao,hali iliyowapelekea kuanguka eneo hilo.Vijana hao walikamatwa na pikipiki yao ikachomwa moto.
 Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo,akiwasimulia watu waliofika kwenye tukio hilo namna mambo yalivyokuwa mpaka kufikia kuchomwa moto kwa pikipiki hiyo yenye nambari za usajili T 636 CXX.
 Taswira za kuwaka moto kwa pikipiki hiyo zikiendelea kuchukuliwa.
 Mdau akijipatia Selfie mbele ya pikipiki iliyokuwa ikiteketea kwa moto wakati huo.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment