MOTO MKUBWA KATIKA YA JIJI LA DAR ES SALAAM NI MTAA WA MOSKI/LIBYA-KARIAKOO

Moto Mkubwa umezuka mapema leo kwenye moja ya nyumba pichani iliopo mtaa wa Moski na Libya-Kariakoo jijini Dar,na kupelekea mali kadhaa kuteketea.Kikosi Kazi cha Globu ya Jamii kipo eneo la tukio kwa sasa kikiendelea kukusanya kila kinachojiri,lakini kwa taarifa kutoka kwa mashuhuda waliopo eneo la tukio wanaeleza kuwa chanzo cha moto huo bado hakijafahamika rasmi,Jeshi la Polisi limefika eneo la tukio kuhakikisha amani na utulivu vinakuwepo huku magari ya zimamoto nayo yakiendelea kuwasili kupambana na moto huo..
Mmoja wa wapiga picha akitazama kwa mshangao moto mkubwa uliokuwa ukiendelea kuwaka kwa nguvu na kuteketeza baadhi ya mali zilizomo ndani ya jengo hilo lililopo mtaa wa Moski/Libya-Kariakoo jijini Dar.
 Baadhi ya Polisi kutoka Jeshi la Polisi na Kikosi cha Zimamoto vikiwasili eneo la tukio.
 Baadhi ya wasamaria wema wakiondoa gari iliokuwa jirani na jengo linaloteketea kwa moto
 Baadhi ya Polisi kutoka Jeshi la Polisi wakiwa katika eneo la tukio,huku wananchi nao wakishuhudia tukio hilo la kusikitisha.
Moja ya Gari ya zimamoto likiwa limewasili eneo la tukio hivi punde.
TUTAWALETEA HABARI KAMILI NA YALIYOJIRI
 KATIKA TUKIO HILO  .
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment