Bao la shuti kali la aina yake la Yaya Toure, moja la Gervinho na jingine la Kanon ndiyo ushindi wa mabao matatu ulioivusha Ivory Coast hadi fainali ya Afcon baada ya kuichapa DR Congo kwa mabao 3-1.
Mechi hiyo ilikuwa ngumu lakini ya kuvutia na DR Congo ilionyesha upinzani mkubwa mkubwa.
Hata hivyo kupaa kwa kiwango cha Ivory Coast, kulichangia kumaliza ndoto za DR Congo kutinga fainali.
Licha ya Rais Joseph Kabila kusafiri hadi Equatorial Guinea kuwaunga mkono vijana wake, lakini waliambulia kupata bao moja tu la Mbokani.
Sasa Ivory Coast inasubiri mshindi kati ya Ghana dhidi ya wenyeji Guinea ambayo inatarajiwa kuwa mechi ngumu licha ya kuwa Ghana ndiyo wanaopewa nafasi ya kukutana na vigogo wenzao kutoka Afrika Magharibi.

0 comments:
Post a Comment