Hiki ndicho walichokisema
makocha David Moyes wa Manchester United, na Arsene Wenger wa Arsenal baada ya
klabu zao kutoka sare tasa kwenye uwanja wa Emirates:
MOYES:
"Nimefurahi,
lakini nilitaka alama zote tatu. Arsenal wana masimu mzuri, hivyo sio sare mbaya
kwetu.
"Nemanja
Vidic na Rio Ferdinand walikuwa wazuri sana uwanjani. Walionesha uzoefu wao
wote.
"Sitaki
kuzungumzia bahati. Lakini wakati fulani hutokea”.
ARSENE WENGER:
"Kwa ujumla
tulitakiwa kushinda. Ilikuwa mechi yenye nafasi chache.
"Umakini
wetu wa kulinda ulikuwa mkali kwa sababu tuliruhusu magoli mengi katika mechi
ya Jumamosi. Mwisho upande mmoja ungewesha kunda 1-0.
"Manchester
United ni timu nzuri, hivyo unapokwenda mbele wanaweza kukukamata.
"Ni muhimu
kujiimarisha zaidi na kujiandaa kwa ajili ya mechi ijayo. Tunataka kubaki katika
kombe la Ligi.
"Kwa kweli
ubingwa unagombaniwa na timu nyingi na mojawapo inaweza kuunyakua."

0 comments:
Post a Comment