Rais Jakaya
Kikwete amemtuma msaidizi wake maalumu, Profesa Mark Mwandosya, kwenda Kigali
katika wakati ambapo uhusiano wa kidplomasia baina ya nchi hizi mbili umekuwa
ukiyumbayumba.
Taarifa ya Ikulu imesema
kuwa Prof Mwandosya, ambaye ni Waziri wa nchi katika ofisi ya Rais, asiyekuwa
na wizara maalumu, aliondoka siku ya Jumamosi na atakuwa nchini Rwanda kwa
zaira ya rasmi itakayodumu kwa muda wa wiki nzima ‘kuona jinsi Rwanda inavyopanga
na kutekeleza huduma za kijamii na kiuchumi’.
Tanzania na
Rwanda zimekuwa katika uhusiano usioridhisha kutoka na ushauri uliotolewa na
Rais Kikwete mwezi Mei mwaka jana kuwa Rwanda ifanye mazungumzo na waasi wa
FDLR kama sehemu ya juhudi za kukomesha mgogoro wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo. Rwanda ilikasirishwa na ushauri huo na kusema moja kwa moja kuwa
hawawezi kukaa meza moja na wauaji. Marais wa nchi hizi mbili – Kikwete na
Kagame- walikutana mwezi Agosti mwaka jana mjini Kampala na kufanya mazungumzo
juu ya suala hilo.
CHANZO: the
Citizen

0 comments:
Post a Comment