Bunge maalum la katiba limemchagua Mh. Pandu Ameir Kificho kuwa mwenyekiti wa muda wa bunge hilo huku baadhi ya wajumbe wakilalamikia kitendo walichokiita ujanja wa serikali wa kuchelewesha kwa makusudi nakala za kanuni za kuendesha bunge la katiba kwa madai ya kuwanyima fursa wajumbe hao kuzipitia kikamilifu ili kuepusha malalamiko na hatimae kupata katiba iliyo bora kwa manufaa ya Watanzania
Mwenyekiti huyo wa muda ambaye ni Pandu Ameir Kificho
amepatikana kutokana na nafasi hiyo kuombwa na wajumbe wanne ambao ni Mh Pandu
Amri Kificho,Magdalena Rubangula na Prof Costa Ricky Mahalu na kupata fursa ya
kujieleza na kuulizwa maswali kadhaa na wajumbe na baadae wajumbe hao kupata
fursa ya kupiga kura ya kumchagua mwenyekiti huyo aliyetangzawa na katibu wa
bunge.
Awali kabla ya kuanza kwa zoezi la kupiga kura ya mwenyekiti wa muda katibu
wa baraza la wawakilishi Zanzibar Yahaya
Hamis Hamad alisoma tangazo la rais la kuitisha
bunge maalum la katiba kuashirika kwamba vikao vya bunge hilo vimeanza
rasmi.
Mapema asubuhi
wajumbe hao wa bunge maalum la katiba wamepata maelekezo ya ukaaji na
jiografia ya ukumbi na baadae kupata fursa kuuliza maswali na kutoa michango
mbalimbali ambapo baadhi ya wabunge wametaka uwepo wa usawa wa jinsia katika
uongozi wa bunge hilo na wengine kutaka kupata kanuni za kuendesha bunge hilo
ili waweze kutoa michango iliyo bora.
Nje ya ukumbi wa bunge tofauti na mabunge mengine katika
bunge hili maalumu la katiba ulinzi uliimarishwa
maradufu ambapo vikosi vya polisi wa doria pamoja na vikosi vya mbwa na farasi
vilikuwa vikirandaranda katika kila kona ya eneo la ndani na nje ya uzio wa
bunge
0 comments:
Post a Comment