Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 31 pamoja na mwanaume mwenye umri wa miaka 19, wamepewa adhabu ya kifungo gerezani mjini Dubai baada ya kukutwa wakipigana busu nyuma ya msikiti mmoja wakiwa ndani ya gari iliyofungwa kwa vioo vyeusi.
Gazeti la Gulf News limeripoti kuwa wapenzi hao walipewa adhabu ya kifungo cha mwezi mmoja baada ya kukutwa na mpita njia aliyewaripoti polisi.
mpita njia huyo alinukuliwa akisema kuwa wapenzi hao "hawakufanya mapenzi lakini nakiri kuwa walikuwa wakipigana busu."
Maelezo zaidi kuhusu kadhia hiyo, tembelea hapa: http://gulfnews.com/news/gulf/uae/courts/court-gives-kissing-couple-one-month-sentences-1.1217432#.UgEdQIN3QUw.twitter
0 comments:
Post a Comment