MAELFU YA WAAGENTINA WAFANYA MAANDAMANO DHID YA SERIKALI

 


Maelfu ya raia wa Agentina wameingia mitaani katika mji mkuu wa nchi hiyo kuonesha upinzani wao dhidi ya mfumko wa bei na ufisadi, ikiwa ni muda mfupi kabla ya ya uchaguzi wa bunge unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Waandamanaji hao walikusanyika katika medani ya Obelisk mjini Buenos Aires na kisha kuelekea kwenye medani ya Plaza de Mayo iliyopo mbele ya jengo la serikali la Casa Rosada.

“Ufisadi unaua kwa sababu tuna hospitali chache, usalama usiotosha na elimu dhaifu, unaua kwa sababu watoto wetu wanakosa ulinzi. Kila kitu kinachochukuliwa na hawa watu kinapaswa kutumiwa kwa ajili ya kuendeleza nchi yetu,” alisema mmoja wa waandamanaji.

Sekta binafsi imetoa tathmini yake na kueleza kuwa kiwango cha mfumko wa bei kimefikia asilimia 25.

Aidha, walionesha hasira yao kwa kuishutumu serikali kujaribu kuudhibiti mfumo wa mahakama wa nchi hiyo na kubadilisha katiba ili kuandaa mazingira mazuri ya kuchaguliwa upya kwa Rais Cristina Fernandez de Kirchner.




Maandamano hayo ni maandamano ya pili dhidi ya serikali ndani ya miezi minne na yamefanywa siku kadhaa kabla ya Waagentina kuamua vyama na wagombea watakaoshindana katika uchaguzi wa bunge unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment