MABOMU YAITIKISA LEBANON


42 killed, 358 wounded in blasts outside two mosques in Lebanon's Tripoli


Kwa uchache watu 42 wamepoteza maisha na mamia kujeruhiwa katika milipuko iliyotokea miwili iliyotokea jirani na misikiti miwili katika mji wa kaskazini wa Tripoli nchini Lebanon.


Mlipuko wa kwanza ulitokea jirani na msikiti wa al-Taqwa katika Uwanja wa Abu Ali wakati waumini wakiondoka msikitini. Msikiti huo upo jirani na makazi ya Waziri Mkuu anayeondoka madarakani, Najib Mikati. 


Mlipuko wa pili, uliotokea dakika tano baadaye, ulitokea katika Msikiti wa al-Salam katika wilaya ya Mina. Msikiti huo upo jirani na nyumbani kwa mkuu wa zamani wa polisi, Ashraf Rifi.

Duru za kiusalama zinasema kuwa watu kumi na nne, wakiwemo watoto watano, waliuawa katika mlipuko uliotokea jirani na Msikiti wa al-Taqwa, huku vifo zaidi vikiripotiwa katika mlipuko wa pili.


Shirika la Msalaba Mwekundu nchini humo, limesema kuwa kwa uchache watu 500 walijeruhiwa katika mshambulizi hayo ya mabomu ya kutegwa kwenye magari.


Wizara ya Mambo ya ndani ilisema kuwa kilogramu 100 ya zana za milipuko zilitumika katika shambulizi lililotokea nje ya Msikiti wa al-Salam.


Aidha, milipuko hiyo iliyaharibu vibaya magari mengi na kuyavunja majengo kadhaa, huku milio thakili ya risasi ikisikia baada ya milipuko hiyo.


Vuguvugu la Chama cha Hizbullah limelaani mashambulizi hayo yaliyofanywa kwenye misikiti.


Hali ya wasiwasi imetanda mjini Tripoli, mji wenye wakazi wapatao 200,000 na ambao ni mji wa pili kwa ukubwa nchini Lebanon, tangu machafuko yalipoibuka katika nchi ya jirani ya Syria.


Mji huo umeshuhudia makabiliano makali baina ya wanaomuunga mkono na wale wanaompinga Rais wa Syria Bashar al-Assad kwa zaidi ya miaka miwili sasa.

Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment