LUGHA 5 NGUMU ZAIDI KUJIFUNZA


Kujifunza lugha mpya ni jambo zuri sana na lenye kumpa furaha mtu anayejifunza.  Lakini vilevile linaweza kuwa zoezi gumu kweli kweli! Tamaduni mbalimbali hudai kuwa zina lugha ngumu zaidi kuliko tamaduni nyingine, hivyo mtu hubaki kuchanganyikiwa asijue ni ipi lugha ngumu zaidi!

Kuna mambo mbalimbali ambayo huifanya lugha husika kuwa ngumu ukiilinganisha na lugha nyingine, kama vile herufi na sauti zake zinavyochanganya, na jinsi kanuni za kisarufi na uandishi unavyokuwa na mchanganyiko wenye utatanishi.

Baada ya kusema hayo, niseme kuwa hakuna lugha maalumu ambayo ni nyepesi na rahisi kujifunza. Lakini kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, na kutokana pia na uzoefu wangu katika kuzungumza lugha nyingi, lugha tano zifuatazo zimeonekana kuwa ndio lugha ngumu zaidi duniani.

Kiarabu

Baadhi ya watu wameiweka lugha hii katika orodha ya lugha ngumu zaidi duniani, kwanza kabisa kwa kuangalia herufi zake zilivyo inaonesha kuwa ni lugha ngumu, hususan kwa wale ambao lugha zao hazishabihiani na lugha hiyo. Mbali na hilo, sababu kubwa ambayo watu wanadhani kuwa inachangia ni kuwa, maneno mengi hayashabihiani nay ale yanayozungumzwa katika lugha nyingine maarufu kama vile Kiingereza na lugha za Ulaya.  Katika lugha ya Kirabu kuna  irabu chache ukilinganisha na lugha nyingine na hili linaifanya kuwa ngumu kwa watu wengi kusoma na kuzungumza lugha husika.

Kichina

Inaelezwa kuwa kwa sasa Kichina ni miongoni mwa lugha muhimu sana hasa kutokana na ukweli kwamba China inelekea kuipiku Marekani katika masuala ya Uchumi wa dunia na kuifanya lugha hii kuwa muhimu sana katika mawasiliano ya kibiashara. Hata hivyo, watu wengi wanasema kuwa ni lugha ngumu kujifunza. Sababu kuu ni kwamba ni lugha ya toni na vokali. Lugha ya toni ni lugha ambayo maana yake hubadilika pale toni ya neno inapobadilika. Aidha, alfabeti za Kichina zina maelfu ya maumbo ambayo huufanya mfumo wa uandishi kuwa mgumu sana.

Kikorea

Lugha nyingine ngumu ni Kikorea. Kwa nini lugha hii ni ngumu kujifunza? Miongoni mwa sababu ni kwamba lugha hii ina uhusiano na matatizo yanayopatikana katika lugha ya Kichina. Unapoandika Kikorea unatumia maumbo mengi magumu mno kama yanayotumika katika lugha ya Kichina. Vilevile, muundo wa sentensi ni mgumu sana, sintaksi zake ni ngumu kuzielewa na minyumbuliko ya vitenzi vyake ndio unakuwa mgumu mno kiasi kwamba si rahisi kujifunza lugha hiyo kwa muda mfupi.


Kijapan

Ni dhahiri kuwa lugha kadhaa za bara la Asia katika orodha yangu hii zimeshika nafasi kubwa katika orodha ya lugha ngumu zaidi kujifunza! Kijapan ni kama Kichina kwa maana kwamba wale wanaojifunza lazima watakutana na suala la maumbo mengi ya herufi. Kijapan ni kigumu zaidi kujifunza kutokana na ukweli kwamba kuna mifumo mitatu tofauti ya uandishi na aina mbili za mifumo ya silabi.

Kihangari

Lugha nyingine ngumu ni Kihangari. Sababu ni kwamba lugha hii ina minyumbuliko saba tofauti ya kitenzi na aina tatu za jinsia. Jambo lingine la kushangaza kuhusu lugha hii ni kwamba halina asili maalumu. Haihusishwi na asili ya lugha nyingi kama Kilatini, ambacho lugha kama vile Kiitalia, Kihispania na Kifaransa zinatoka huko.

USHAURI
Kama unataka kujifunza lugha yoyote katika ya hizo tano, usikatishwe tamaa na hayo niliyoyaeleza. Kitu kuwa kigumu haina maana kwamba hakiwezekani. Aidha, uchughuzi huu unaweza usiwahusu watu wote. baadhi ya watu huwa wanajifunza mambo kwa urahisi zaidi. Hivyo, piga moyo konde na ujipange, ninaamini huwezi kushindwa kujifunza!


Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment