UTURUKI: MAPINDUZI YA MISRI NI MAPINDUZI "HARAMU"

Turkish Prime Minister Recep Tayyip Erdogan (R) and ousted Egyptian President Mohamed Morsi
Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan (kulia) na aliyekuwa Rais wa Misri Muhamamad Mursi


Waziri Mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, ameelezea upinzani wake mkubwa dhidi ya mapinduzi ya kijeshi nchini Misri yaliyomuondoa aliyekuwa rais wa nchi hiyo  Muhammad Mursi, akiita hatua hiyo kuwa 'haramu.'

Akielezea matukio ya hivi karibuni nchini Misri jana Alhamisi, Erdogan alisema kuwa Uturuki inayachukuliwa mapinduzi hayo kuwa "haramu," shirika rasmi la habari la Anadolu liliripoti. 

“Kila mapinduzi ya kijeshi, bila kujali malengo, nchi na sababu yake, ni unyongaji wa demokrasia, watu na mustakbali wa nchi," Erdogan alisema na kuongeza kuwa maandamano ya kuipinga serikali mjini Cairo hayakuhalalisha mapinduzi hayo.

Misri ilitumbukia katika machafuko na ghasia baada ya jeshi kumuondosha Mursi, kusitisha matumizi ya katiba, na kulivunja bunge mnamo Julai 3. Jeshi lilichukua hatua hiyo kufuatia siku kadhaa za maandamano ya kumpinga Mursi.

Tarehe 4 Julai jeshi lilimtangaza mkuu wa Mahakama Kuu ya Katiba, Adly Mansour, kuwa rais wa mpito.

Wziri Mkuu huyo wa Uturuki aliongeza kuwa, “iwapo viwanja ndio dalili, vipi kuhusu uwanja wa  Rab’a Al-Adawiya?” akimaanisha uwanja ulio jirani na makao ya rais wa Misri, ambapo wafuasi wa Mursi walikuwa amekusanyika.

Julai 5, Erdogan alilaani hatua ya kuondolewa Mursi madarakani kwa jeshi kuingilia kati na kuzikosoa nchi za Magharibi kuwa kushindwa kuiona hatua hiyo kuwa ni mapinduzi.

Tangu wiki jana, Misri imekuwa ikishuhudia maandamano na makabiliano yanayowahusisha wafuasi na wapinzani wa Mursi na vikosi vya usalama. Watu wengi wameuawa kwa siku kadhaa zilizopita huku zaidi ya watu 80 wakiripotiwa kuuawa Julai 8 pekee.

Julai 10, serikali ya Misri inayoungwa mkono na jeshi ilishadidisha mbinyo dhidi ya chama cha Muslim Brotherhood, kwa kutoa amri ya kukamatwa kwa kiongozi wake wa kiroho, Mohamed Badie na maafisi wengine waandamizi.


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ameelezea wasiwasi wake kuhusu kushikiliwa kwa wanaharakati wa kisiasa nchini Misri na kusema kuwa, “kufanya ubaguzi kwa  chama au jamii yoyote ni jambo lisilokubalika.”
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment