
Mwamuzi mmoja wa soka amechinjwa na watazamaji kufuatia mgogoro uliopelekea mwamuzi huyo kumjeruhi vibaya mchezaji mmoja aliyekataa kutoka uwanjani.
Msemaji wa jeshi la Polisi nchini Brazili, Kena Souza alisema jana Jumamosi kuwa tukio hilo lilitokea Juni 30 katika mji mdogo wa kaskazini wa Pio XII.
Mzozo huo ulianza baada ya mchezaji Josenir dos Santos (miaka 30) kumtukana na kumkaripia mwamuzi Octavio da Silva, akipinga hatua yake ya kumpa kadi nyekundu.
Mzozo huo ulianza baada ya mchezaji Josenir dos Santos (miaka 30) kumtukana na kumkaripia mwamuzi Octavio da Silva, akipinga hatua yake ya kumpa kadi nyekundu.
inasemekana kuwa Dos Santos alimpiga ngumi da Silva, naye akatoa kisu na kumjeruhi mchezaji huyo.
Watazamaji walikasirishwa na kitendo cha refa huyo, wakavamia uwanja na kumpiga mawe kabla ya kumkata kichwa.
Souza alisema kuwa mnamo Julai 2 polisi ya mkoa wa Santa Ines walimtia mbaroni mtu mmoja kwa mauaji hayo na mamlaka zinaendelea kulichunguza tukio hilo.
Shumbilio hilo la aina yake linatokea wakati Brazil inapambana kuhakikisha inakuwa nchi salama kabla ya kuandaa mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2014 na michuano ya Olimpiki mwaka 2016.
Michuano ya hivi karibuni ya Kombe la Mabara, ambayo ilifanyika nchini humo mwezi Juni, ilitawaliwa na ghasia wakati polisi wakihaha kutuliza maandamano ya kupinga hatua ya serikali kutumia kiasi kikubwa cha pesa kuandaa mashindano hayo.
CHANZO: PRESS TV
0 comments:
Post a Comment