Binti mmoja wa Kimisri mwenye umri wa miaka 15 aliyekataa shinikizo la familia yake kumtaka avae vazi la Kiislamu, yaani hijabu, alijipiga risasi kwa kutumia bastola ya baba yake, tukio hilo limeripotiwa na vyombo vya habari vya Misri na eneo zima la Mashariki ya Kati.
Tukio hilo la kujiua, lililotokea wiki iliyopita huko katika wilaya ya Giza, liliripotiwa na tovuti maarufu ya habari nchini humo ijulikanayo kama Youm7.
Binti huyo aliyetambulika kwa jina la Amira, anaelezewa kupata msukosuko kutoka kwa familia yake baada ya kuondosha hijabu yake.
Kwa mujibu wa tovuti hiyo, uchunguzi uliofanywa ulibaini kuwa kutokana na hali hiyo, Amira aliamua kuingia ndani na kuchukua silaha ya baba yake na kujiua.
CHANZO: al Arabiya
0 comments:
Post a Comment