![]() |
Muasisi wa Mapinduzi ya Jamuri ya Kiislamu ya Iran, hayati Ayatollah Seyyed Rouhollah Khomeini |
Iran inaadhimisha kumbukumbu ya miaka 24 ya kifo cha muasisi wa Jamhuri hiyo ya Kiislamu, Ayatollah Seyyed Rouhollah Khomeini.
Wairan, ndani na nje ya nchi, wanafanya shughuli mbalimbali za maadhimisho ya kifo cha kiongozi huyo, Imam Khomeini.
Idadi kubwa ya watu na maafisa mbalimbali wamekusanyika katika eneo alilozikwa Ayatollah Khomein, kusini mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Tehran kwa ajili ya maadhimisho hayo.
Kiaongzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah Seyyed Ali Khamenei atahutubia hadhara hiyo.
Mjukuu wa Imam Khomeini, Hujjatul Islam Seyyed Hassan Khomeini, naye pia atahutubia.
Kila mwaka, mamilioni ya Wairan nchini kote, hufunga safari kwenda mjini Tehran kutembelea kaburi la kiongozi huyo.
Rouhollah Mousavi Khomeini, aliyekuja kujulikana kama Imam Khomeini, alizaliwa katika mji wa Khomein Septemba 24, 1902.
Kiwa ametokana na familia ya wanazuoni, kijana Rouhollah alianza masomo yake kwa kuhifadhi Qur'an Tukufu na baadaye akaenda Arak (1920-21) na Qum (1923) kukamilisha masomo yake ya kidini.
Miaka ya 30, Imam Khomeini alijitolea muda wake kufundisha sheria ya Kiislamu mjini Qum.
Mwaka 1961, Ayatollah Khomeini alikuwa chanzo cha marejeo ya mafunzo ya madhehebu ya Kishia na taratibu akaanza kuingia katika medani ya kisiasa. mnamo Januari 1963, alijihusisha moja kwa moja katika harakati dhidi ya mfalme wa Iran wa wakati huo, Mohammad-Reza Pahlavi, ambaye alikuwa ametangaza programu yake aliyoiita: Mapinduzi Meupe.
Imam Khomeini alibadilisha maisha ya Wairan na kuwapa hamasa watu kutoka nchi mbalimbali kwa kuongoza mojawapo ya mapinduzi makubwa kabisa katika historia ya zama za sasa na kupata ushindi.
Ayatollah Khomeini alifariki dunia Juni 3, 1989, siku 11 baada ya kupelekwa hospitalini kwa ajili ya kufanyiwa oparesheni ya kuzuia tatizo la kuvuja damu mwilini mwezi Mei 1989.
Baada ya kifo cha Imam Khomeini, Ayatollah Seyyed Ali Khamenei alichaguliwa na Jopo la Wataalamu kuwa kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
MAKALA HII IMEANDALIWA NA TIMU YA MZIZIMA 24 KWA MSAADA WA MTANDAO.
0 comments:
Post a Comment