Vijana CUF sasa watishia Serikali



Dar es Salaam. Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Wananchi (JUVICUF), imetishia kuandamana nchi nzima ikiwa haki haitatendeka kwa mwenyekiti wao, Katani Ahmed Katani aliyekamatwa na na polisi kwa tuhuma za uchochezi mkoani Mtwara.
Mwenyekiti huyo, alikamatwa Alhamisi Dar es Salaam na kusafirishwa kwa ndege kwenda mkoani Mtwara, ambako vurugu zilizotokea kupinga ujenzi wa bomba la kusafirishwa gesi kwenda jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa JUVICUF, Yusufu Kaiza aliwaambia akisema “Tunataka atakapofikishwa mahakamani apewe dhamana na kama tukiona haki haitendeki juu yake, sisi tutaitisha maandamano nchi nzima kuhakikisha haki inatendeka’’.
Kaiza alisema Serikali inatakiwa kukutana na wananchi wa Mtwara na kuzungumza nao kwa undani juu ya manufaa watakayoyapata kutokana na mradi wa gesi asilia na siyo kuanza kukamata watu ovyo.
Alisema Katani alikamatwa Alhamisi baada ya kupigiwa simu na maofisa wa polisi wa Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam na alipofika aliwekwa chini ya ulinzi na kuhojiwa kwa saa kadhaa.
“Katani anakubalika sana mkoani humo kutokana na kujulikana sana kisiasa kwani mwaka 2010 aligombea Ubunge Jimbo la Tandahimba na kushindwa kwa mizengwe’’, alisema Kaiza.

CHANZO: Mwananchi
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment